Mapinduzi Cup

Tanzania Bara na Visiwani kukiwasha leo Gombani

PEMBA: MICHUANO ya Kombe la Mapinduzi inaanza leo kwa mechi ya ufunguzi kati ya wenyeji timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes na Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Uwanja wa Gombani, Pemba.

Mchezo huo utakuwa ushindani mkubwa kutokana na makocha wa timu hizo kufahamiana, kwa Zanzibar Heroes inanolewa na Hemed Morocco ambaye ni kaimu kocha mkuu wa Taifa Stars huku Kilimanjaro Stars ikinolewa na Ahmad Ally.

Kuelekea mchezo huo Kocha Msaidizi wa Zanzibar Heroes, Ali Suleiman Mtuli, amesema wanategemea kuwa na mechi kubwa kwa sababu Zanzibar Heroes na Kilimanjaro Stars ni ndugu.

“Tunajua itakuwa ni mechi ngumu, lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata ushindi siku ya leo , mechi yetu dhidi ya Tanzania Bara haijawahi kuwa rahisi kuanzia mashabiki hadi wachezqji, “ amesema

Kocha mkuu wa Kilimanjaro Stars, Ahmad Ally amesema moja ya malengo yao ni kufanya vizuri kwa kushinda mechi dhidi ya Zanzibar Heroes.

“Itakuwa mechi ya kiufundi sana kwa sababu ya kocha wao (Morocco) tunafahamu ubora wake kiufundi na ubora wa wachezaji aliokuwa nao hasa kwenye safu ya kiungo,” amesema.

Ahmad amesema tumejaribu kuangalia ubora wa Zanzibar ili kufikia malengo ikiwemo kutafuta matokeo katika mchezo dhidi ya Zanzibar Heroes na kupata matokeo chanya.

Related Articles

Back to top button