Squid Game ni vunja weka

SERIES maarufu kwa sasa ya Squid Game season 2 imeweka rekodi ya kuwa series ya kwanza kufikisha watazamaji zaidi ya milioni 60 kwenye mtandao wa Netflix katika wiki yake ya kwanza ya kuachiwa yaani wiki inayoanzia Desemba 26, 2024 Januari Mosi 2025.
Rekodi hiyo hapo awali ilishikiliwa na season ya kwanza ya Series ya Kimarekani iitwayo Wednesday iliyofikisha views milioni 50.1 katika kipindi kama hicho mwezi Novemba mwaka 2022 ilipoachiwa rasmi kwenye mtandao huo huo wa Netflix.
Series hiyo ya Kikorea ambayo imezalishwa chini ya ‘Director’ Hwang Dong-Hyuk inafuata nyayo za season yake ya kwanza ambayo bado ipo kwenye orodha ya Series zilizotazamwa mara nyingi zaidi kwa miaka miwili sasa.
Tayari season 3 ya Squid Game ipo kwenye hatua mbalimbali za uzalishaji na linatarajiwa kuachiwa baadae mwaka huu.