Filamu

Spider-Man ‘Brand New Day’ imeshaingiza trilioni 6.5

NEW YORK: FILAMU ya Spider-Man: Brand New Day, iliyomshirikisha mwigizaji Tom Holland, inatarajiwa kurejea tena katika kumbi za sinema ikiwa na picha mpya ambazo hazikuonekana kwenye toleo la awali.

Kwa mujibu wa taarifa mpya iliyonukuliwa na Hindustan Times, filamu hiyo ambayo tayari imeingiza karibu dola bilioni 2.5, sawa na takribani Shilingi trilioni 6.5 za Tanzania, duniani kote, inaweza kuoneshwa tena kabla ya kumalizika kwa mwaka 2026.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa toleo jipya litakuwa na picha za ziada, ingawa Marvel Studios na Sony Pictures bado hazijatangaza rasmi tarehe ambayo filamu hiyo itarejea kwenye sinema.

Spider-Man: Brand New Day ilianza kuoneshwa duniani Julai 31, 2026 na imekuwa miongoni mwa filamu zilizofanya vizuri zaidi katika historia ya sinema, huku mapato yake ya kimataifa yakifikia karibu dola bilioni 2.5.

Nchini Marekani na Canada, filamu hiyo imekusanya takribani dola milioni 950.6, sawa na zaidi ya Shilingi trilioni 2.4 za Tanzania, ikiwa ni moja ya filamu zilizofanya vizuri zaidi katika soko hilo.

Iwapo itarejea kabla ya Desemba, toleo hilo linaweza pia kuongeza hamasa kuelekea filamu ijayo ya Marvel, Avengers: Doomsday, ambayo inatarajiwa kumrejesha Robert Downey Jr. katika ulimwengu wa Marvel.

Related Articles

Back to top button