EPLKwingineko

Son: Hasira ilituchochea

MSHAMBULIAJI wa Tottenham Hotspur, Son Heung-min, amekiri timu yake ilisawazisha mabao dhidi ya Manchester United Aprili 27 kutokana na hasira ya kuwa nyuma 2-0 siku chache tu baada ya kubamizwa mabao 6-1 na Newcastle.

United ilitangulia kupata mabao katika mchezo huo wa Ligi Kuu England(EPL) kupitia Jadon Sancho na Marcus Rashford lakini Spurs iliimarika kipindi cha pili ikisawazisha kuwa 2-2 mabao yakifungwa na Pedro Porro na Son Heung-min.

“Hatukutaka kupoteza mchezo. Tulikasirishwa sana na hilo, hatukustahili kuwa nyuma kwa mabao 2-0 hadi mapumziko,” amesema Son.

Tottenham inashika nafasi ya 5 katika msimamo wa EPL ikikusanya pointi 54 huku ikiwa imebakiza mechi 5 kabla ya ligi kufikia tamati.

Related Articles

Back to top button