Ligi Kuu
Simba yapigwa faini Sh milioni 1
SIMBA SC imetozwa faini ya Sh milioni 1 kwa kosa la mashabiki wake pamoja na walinzi wake kufanya vitendo vinavyoashiria imani za kishirikina katika mchezo dhidi ya Mashujaa FC.
Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu imesema imewafungia mwaka mmoja walinzi na shabiki waliohusika kuingia uwanjani, huku uchunguzi ukiendelea kubaini wengine.
Kamati hiyo imesema adhabu hiyo imezingatia kanuni ya 47:1 ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti wa klabu.