Africa
Simba Queens kutinga nusu fainali?

TIMU ya soka ya wanawake Simba Queens inashuka uwanjani leo dhidi ya Green Buffaloes katika mchezo wa mwisho wa kundi A michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake inayoendelea Morocco.
Simba Queens inahitaji ushindi katika mchezo huo katika uwanja wa Grand De Marrakech ili kufuzu.
Timu hizo zina pointi pointi 3 kila moja ingawa Buffaloes ni ya pili na Simba Queens ya tatu hivyo klabu yoyote itakayoshinda itafuzu nusu fainali.
FAR Rabat Women inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi 6.