Simba kuingia kambini wiki ijayo

DAR ES SALAAM: KIKOSI cha Simba SC kinatarajiwa kuingia kambini wiki ijayo kwa maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Bigman, utakaopigwa Machi 27 kwenye Uwanja wa KMC Complex, Mwenge.
Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema kuwa wachezaji waliopo kwenye majukumu ya timu za taifa wataendelea na majukumu yao, huku wale wasiohusika wakipewa mapumziko mafupi kabla ya kurejea kambini.
“Baada ya mchezo wetu dhidi ya Bigman kwenye Kombe la CRDB, Machi 27, tutasafiri Machi 28 au 30 kuelekea Misri kwa ajili ya mchezo wa robo fainali ya CAF dhidi ya Al Masry,” amesema Ahmed.
Ameongeza kuwa wachezaji waliopo kwenye timu za taifa watajiunga na wenzao mara baada ya kumaliza majukumu yao, maandalizi yakiendelea kwa michezo muhimu iliyopo mbele yao, ikiwemo michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.




