Africa
Al Ahly yawasili kuikabili Simba
KIKOSI cha timu ya Al Ahly ya Misri kimewasili nchini tayari kuikabili Simba katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi Mabingwa Afrika.
Mchezo huo utafanyika Machi 29 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam wakati marudiano yatakuwa Aprili 5 Cairo, Misri.
Klabu ya Simba imekuwa ikifanya hamasa kuelekea mchezo huo iliyopewa kauli mbiu, ‘Tunaitaka nusu fainali, Tukutane kwa Mkapa.’