Ligi Kuu

Simba kuifuata Pamba usiku wa manane

DAR ES SALAAM: KIKOSI cha Simba kinaondoka  Dar es Salaam leo usiku kuelekea Mwanza kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Pamba Jiji FC, utaopigwa Novemba 22, Uwanja wa CCM Kirumba.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally katika uzinduzi wa jezi watakazovaa katika michezo ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Amesema kikosi kinaendelea na program ya mazoezi kikijiandaa dhidi ya Pamba Jijini FC, ugenini.
“Leo usiku tutaondoka kwenda Mwanza na wachezaji wanne waliokuwa Stars, Moussa Camara aliyekuwa Guinea ameshajiunga na kambi na Steven Mukwala  atawasili Dar es Salaam Alhamisi Novemba 21 na kuunganisha kwenda Mwanza,” amesema.

Ahmed ameongeza kuwa kesho watakuwa Mwanza na kutembelea kituo cha watoto Yatima cha Ilemela kurudisha kwa jamii. Mchezo dhidi ya Pamba ni muhimu mno kushinda sababu utawapa ujasiri kuelekea mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Bravos do Maquis ya Angola.

“Nichukue nafasi hii kuwaambia mashabiki wetu wa Mwanza na Kanda ya Ziwa kwamba waangalie Pamba kama mpinzani wetu mgumu kwa maana hiyo wafanye maandalizi makubwa ya kwenda kumuangamiza Pamba, tunahitaji ushindi,” amesema.

Ahmed ameeleza baada ya mchezo dhidi ya Pamba usiku huo huo wa Ijumaa Novemba 22 wataondoka kurejea Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Bravos do Maquis.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button