Burudani
Mobetto unajikubali wewe!.. hiyo shepu vipi?
DAR ES SALAAM: Mwanamitindo, Hamisa Mobetto amesema kuwa hajawahi kufanya upasuaji wa kutengeneza umbo lake kwani ameridhika na jinsi alivyo.
Akizungumza na SpotiLeo Hamisa amejigamba kuwa mwili aliokuwa nao mwanzo ndio alionao sasa.
“Nadhani watu wanapaswa kujua tofauti ya miili ya asili na miili ya upasuaji sijawahi kufanya ila hapo baadae umri ukienda nikihitaji kufanya upasuaji nitafanya na mtaona.”amesema Hamisa
Ameongeza kuwa anaupenda mwili wake kwani haumkwamishi kufanya kitu chochote yuko sawa na anafanya vitu vingi ikiwemo ubunifu wa mavazi.
Katika hatua nyingine Hamisa amefunguka sababu ya kutokuonekana tena kwenye muziki ambapo amesema amesema ameamua kujipa muda wa kulea familia yake.
Mrembo huyo amesema kwa sasa anaendelea na kazi zake hivyo hatoweza kujihusisha na muziki hadi atakapomaliza .
“Muda mwingi nimekuwa katika project zangu muda wa kufanya muziki nikosa hivyo nimejipa muda hadi hapo nitakapo wataarifu, kwa muziki unahitaji muda nami kwa sasa sina muda nipo na kazi nyingi na nitaendelea na project zangu sitaki kufanya muziki,” amesema Mobetto.