Africa

Serikali yateta na Simba, Yanga

DAR ES SALAAM: KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa amesema wamekutana na viongozi wa  Simba na Yanga kuelekea katika michezo yao ya Kimataifa wikiendi hii.

Yanga inaiwakilisha nchi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe, Lubumbashi nchini DR Congo Desemba 14 na  Desemba 15 Simba kucheza kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam dhidi ya CS Sfaxien.

Msigwa amesema wanaendelea kuwaunga mkono kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye michezo yao ijayo, walikutana viongozi hao kuzungumza baada ya kurejea nchini wakitokea Algeria.

“Tulizungumza na viongozi wa klabu hizi mbili na wamepeleka maelekezo ya bechi lao la ufundi kufanya kazi makosa yaliyojitokeza na kuhakikisha kwenye michezo ya wikiendi hii tunafanya vizuri.

Yanga watakuwa ugenini dhidi ya TP Mazembe lakini Simba nao wako nyumbani tutakuwa nao Uwanja wa Benjamin Mkapa wote tunawatakia kheri na tunaimani timu hizi zitafanya vizuri na kusonga mbele hatua ya robo , nusu na fainali, “ amesema.

Msigwa amesema wanaendelea kuwaunga mkono kuhakikisha timu zinafanya vizuri na matarajio yao wikiendi hii Simba na Yanga watafanikiwa kuondoka na fedha za Goli la Mama.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button