Nyumbani

Samatta arejea tena Taifa Stars

KAIMU Kocha wa timu ya Taifa Stars, Hemed Morocco ametangaza kikosi cha timu hiyo ch wachezaji 23 huku akimerejesha Mbwana Samatta pamoja na kujumisha sura mpya akiwemo beki wa Simba Abdulrazack Hamza.

Wengine wapya ni mshambuliaji wa Fountain Gate FC, Suleman Mwalimu, Nassor Saadun (Azam FC) na Abdallah Said (KMC FC) kwa ajili ya michezo miwili ya kuwania Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya DR Congo.

Morocco amesema kikosi kinatarajia kuingia kambini Oktoba 4 . Mchezo wa kwanza utapigwa Oktoba 10 ugenini na kisha nyumbani Oktoba 15.

“Kelvin John tunaendelea kumfatilia na Samatta amerudi kikosini kulingana na mechi zilizopo mbele yetu, nimewafatilia wachezaji na ligi ambayo wanacheza wachezaji watanzania wapo wazuri lakini inategemea nafasi na mechi tunazoenda kucheza,” amesema Morocco.

Kuhusu makipa amesema Tanzania imekuwa na changamoto ya makipa lakini Ally Salim amecheza vizuri katika michezo miwili na kigezo kikubwa ambacho kimeendelea kumuita tena.

Wachezaji wengine ni Ally Salim, Mohammed Hussein, Kibu Denis (Simba), Zuberi Foba, Lusajo Mwaikenda Pascal Msindo, Adolf Mtasigwa, Feisal Salum na Saaduni (Azam FC).

Wengine ni Yona Amos (Pamba)Ibrahim Bacca, Bakari Mwamnyeto, Mudathir Yahya, Clement Mzize (Yanga), Haji Mnoga (Salford City, Uingereza), Habib Khalid (Singida Black Stars) na Cyprian Kachele (Vancouver Whitecaps, Canada)

Related Articles

Back to top button