Burudani

Sam Pounds afunguka mazito

LONDON: Mtayarishaji Sam Pounds ameamua kuchelewesha kutolewa kwa wimbo wa Liam Payne, unaoitwa “Do No Wrong,” baada ya awali kutangaza kuuachia Novemba 1, Ijumaa ya Jana.

Mtayarishaji huyo aliingia kwenye mitandao ya kijamii Oktoba 29 ili kutoa uamuzi wake wa kuachia wimbo huo, akisisitiza kwamba ataacha chaguo hilo kwa wanafamilia wote. Pounds alisema, “Sote bado tunaomboleza kifo cha Liam na ninataka familia kuomboleza kwa amani na katika maombi.”

Pounds awali alionesha matumaini ya kuachia wimbo huo aliodai utakuwa baraka kwa familia ya Payne na mashabiki, akimtaja dada wa Payne, Ruth, na mwanawe, Bear.

Mtayarishaji huyo alidokeza kwamba alitamani mapato kutoka kwa wimbo huo yangefaidisha familia ya Payne. Hata hivyo, Pounds baadaye alielezea kwamba alihisi kwamba amehisi si wakati sahihi kuachia wimbo huo kwa sasa kama baadhi ya mashabiki na wanafamilia walivyotoa maoni yao baada ya tamko lake la kuachia wimbo huo Novemba 1.

Payne alipatikana akiwa amekufa Oktoba 16 katika hoteli moja wapo nchini Argentina baada ya kuanguka kutoka ghorofa ya tatu.

Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Kitaifa wa Argentina ilisema. Liam Payne aliyekuwa na miaka 31, uchunguzi wa maiti yake umeonyesha majeraha 25 yanayotokana na kuanguka kutoka urefu huo na hivyo sababu ya kifo chake imeelezwa kuwa ni kutokwa na damu nyingi ndani na nje ya mwili

Related Articles

Back to top button