Kwingineko

Carsley akitamani kibarua cha Tuchel

LONDON: Meneja wa zamani wa muda wa timu ya taifa ya England, Lee Carsley amesema anatamani kupata tena fursa ya kuinoa timu hiyo wakati huo akiendelea na majukumu yake kwenye kikosi cha timu ya vijana ya U21 inayojiandaa kutetea ubingwa wa Ulaya.

Carsley amekiambia chombo kimoja cha habari nchini England kuwa akiwa na timu hiyo ya wakubwa huwa anajisikia raha na kuona ni mtu muhimu zaidi kuliko akiwa kwenye majukumu yake ya sasa.

“Ni kitu ambacho huwa nafurahia sana kufanya, kama nilivyosema awali ni lazima upambane uwe kwenye nafasi kama ile na mimi nitafanya niwezalo. Najisikia furaha sana huwa naona nimeaminiwa kufanya kazi hii ya sasa lakini ngoja tuone yajayo” amesema Carsley

Meneja huyo mwenye miaka 51 alishinda michezo mitano kati ya sita aliyoisimamia timu ya taifa ya England kama meneja wa muda baada ya kocha wa kikosi hicho cha the three Lions Gareth Southgate kujiuzulu kufuatia kukosa ubingwa wa Euro 2024 mbele ya Hispania.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button