Africa

Rais wa zamani Nigeria hapendi makocha wazawa

LAGOS, Nigeria: RAIS wa zamani wa Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF), Amaju Melvin Pinnick amefichua sababu inayomfanya apende makocha kutoka nje ya nchi kufundisha timu za taifa.

Pinnick ambaye kwa sasa ni mjumbe wa baraza la FIFA, alisema sababu yake ya kuwachukia makocha wazawa inatokana na kutoheshimu wachezaji wanaowaongoza.

“Ndiyo, makocha wa Nigeria wana ujuzi na uwezo wa kiufundi unaohitajika, lakini soka la kisasa ni zaidi ya hilo katika kusimamia wachezaji.

“Je, wachezaji wa timu ya taifa watamheshimu kocha? Jambo la kusikitisha ni kwamba hawafanyi hivyo,” alisema kwenye mahojiano na Arise TV ya nchini humo.

Katika utawala wa Pinnick alimteua Mjerumani, Gernot Rohr kuiongoza Super Eagles kwa muda mwingi wa utawala wake.

Kocha mwingine wa kigeni Randy Waldrum aliteuliwa kuinoa timu ya taifa la wanawake ya nchi hiyo, Super Falcons.

NFF bado inawinda kocha wa kigeni baada ya kuwa na kocha wazawa kwa muda sasa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button