Africa

Stars mtihani leo

TIMU ya taifa ya soka(Taifa Stars) leo inashuka dimbani dhidi ya Algeria katika mchezo wa mwisho wa makundi kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika(AFCON) 2023.

Mchezo huo wa kundi F utafanyika kwenye uwanja wa 19 May 1956 uliopo mji wa Annaba Kaskazini Mashariki mwa Algeria huku Stars ikitakiwa kushinda ili kujihakikishia kufuzu.

Niger itaikaribisha Uganda katika mchezo mwingine wa kundi hilo kwenye uwanja wa Marrakech, Morocco.

Algeria inaongoza kundi F ikiwa na pointi 15 ikifuatiwa na Tanzania yenye pointi 7, Uganda ina pointi 4 wakati Niger iliyopo nafasi ya mwisho ina pointi 2.

Michezo mingine ya kufuzu fainali hizo ni kama ifuatavyo:

KUNDI E
Angola vs Madagascar
Ghana vs Jamhuri ya Afrika ya Kati

KUNDI J
Tunisia vs Botswana

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button