Ligi KuuNyumbani

Polisi Tanzania kuboresha kikosi

TIMU ya Polisi Tanzania itakifanyia maboresho makubwa kikosi chake wakati wa dirisha dogo ikiwemo kusajili wachezaji wa kiwango kikubwa watakaosaidia kuleta matokeo mazuri katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na SpotiLeo Kaimu Kocha Mkuu wa timu hiyo John Tamba amesema pamoja na kuwa Polisi Tanzania ipo nafasi mbaya kwenye msimamo wa ligi, lakini haitashuka daraja kama ambavyo watu wengi wanavyoitabiria.

“Kinachotusumbua ni mapungufu yaliyopo kwenye timu lakini uongozi umenihakikishia kwenye dirisha dogo tutavunja rekodi kwa kufanya usajili wa wachezaji wakubwa na kuiondoa timu kwenye nafasi mbaya iliyopo,” amesema Tamba.

Kocha huyo amesema anatambua presha ni kubwa kwa wakazi wa Kilimanjaro lakini ligi bado ni ndefu na kikosi chake kina nafasi ya kurekebisha mapungufu na kuendelea kushiriki kwenye ligi za misimu inayokuja.

Polisi Tanzania inashika nafasi ya 15 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 9 baada ya michezo 14.

Related Articles

Back to top button