Mexime anyoosha mikono kwa Simba

DAR ES SALAAM: KOCHA Mkuu wa Dodoma Jiji FC, Mecky Maxime, ameweka wazi kuwa Simba SC walikuwa bora na walitumia makosa ya wachezaji wake ipasavyo, hali iliyosababisha timu yake kupokea kipigo kikubwa katika mchezo wao wa kiporo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la KMC Complex, Mwenge jijini Dar es Salaam, Simba SC waliibuka na ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Coastal Union, matokeo yaliyoonyesha wazi ubora wa kikosi cha Wekundu wa Msimbazi.
Maxime alieleza kuwa wachezaji wake hawakuwaheshimu wapinzani wao na walijikuta wakifanya makosa mengi yaliyoigharimu timu. “Hatukuweheshimu Simba, tulifunguka na kutaka kushindana nao, lakini tulifanya makosa mengi ambayo wapinzani wetu walikuwa na uwezo wa kuyatumia kutuadhibu,” amesema kocha huyo.
Hata hivyo, Maxime alisisitiza kuwa Dodoma Jiji FC inarejea mazoezini ili kurekebisha mapungufu yao na kuhakikisha makosa kama hayo hayajirudii katika mechi zijazo. Lengo lao kuu ni kubaki kwenye ligi kwa kuimarisha kikosi na kujifunza kutokana na makosa waliyoyafanya katika mchezo huo.