Nyumbani

Simba: Ukimya wetu una kishindo

DAR ES SALAAM. UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa ukimya wao unakishindo baada ya watu maalum kuingia sokoni kwa kutorejea makosa waliyofanya nyuma katika usajili wa wachezaji wapya.

Imeelezwa kuwa tayari Simba imeshamalinzana na nyota watatu wapya akiwemo Yusuph Kagoma (Singida Fountain Gate FC), Lameck Lawi (Coastal Union) na  Elie Mpanzu (AS Vita Club ya DR Congo).

Akizungumza na Spotileo, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba,  Ahmed Ally amesema tangu ligi imalizike wamekuwa kimya hali ambayo imeleta hofu kwa mashabiki wao .

Amesema usahihi ni kuwa mipango thabiti inaendelea na itakapokuwa tayari wanasimba watafahamu juu ya ukimya waliokuwa nao kwa kipindi chote.

“Jambo la kufurahisha ni kwamba mipango yote inatekelezwa kwa ustadi na ufanisi wa hali ya juu mnoo, malengo tuliyoiweka ya kuboresha timu yetu yamefanikiwa kwa asilimia kubwa kwa maana mipango yetu kwenye soko la usajili iko vizuri.

Niwaombe wanasimba tutulie, la mambo likilia tutafurahi kila kitu kuhusu timu yetu kinaenda sawa , ikiwemo suala la usajili haturudii makosa yaliyojitokeza awali ,” amesema  Ahmed.

Amesema uliopita  ulikuwa ni msimu wenye ushindani mkubwa na matarajio yao yote hayajatimia jambo linalowapa masikitiko na somo kwa msimu ujao wa Mashindano.

“Tuna majonzi makubwa kwa wakati huu ninatambua kwamba Wanasimba hawajafurahi namna ambavyo tumemaliza, haya masikitiko kwetu hatujafikia malengo yetu kwa asilimia kubwa hilo lipo wazi, nyakati zinabadilika  tunaamini kwamba tutarejea tukiwa imara.

Bado tuna muda wakufanyia kazi makosa ambayo yalipita kwa ajili ya kuwa imara wakati ujao, mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi mambo mazuri yanakuja na tutafanya vizuri katika wakati ujao.” Amesema Meneja huyo.

Simba wameshindwa  kufikia malengo yao kwa asilimia kubwa msimu wa 2023/24, ipo wazi kuwa ni namba tatu imegotea kwenye ligi ikiwa na pointi 69 tofauti ya mabao ya kufungwa na kufunga dhidi ya Azam FC iliyomaliza ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo.

Kombe la CRDB Federation Cup imepishana nalo kama ilivyokuwa kwenye taji la ligi katika Ligi ya Mabingwa Afrika iligotea hatua ya robo fainali ikikwama kutwaa taji hilo kubwa Afrika na iliposhiriki African Football Cup iligotea hatua ya robo fainali

Related Articles

Back to top button