PM ataka Taifa Stars ya moto.
DAR ES SALAAM: WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ametaka kufanya mabadiliko ya haraka kwa timu ya taifa ya Taifa Stars iwe na ushindani kwenye mashindano ya mataifa ya Afrika (AFCON), 2027 yatakayo andaliwa kwa pamoja na nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.
Amezungumza hayo katkka halfa ya uzinduzi wa kamati na kukabidhi mpango mkakati wa maandalizi ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON ) 2027, inayosimamiwa na Leodgar Tenga (Mwenyekiti), Ayoub Mohammed (Makamu Mwenyekiti), Katibu ni Neema Msitha na Said Kassim (Katibu Msaidizi).
Waziri Mkuu Kasim Majaliwa amesema maandalizi yaanze mapema kwa kuwashirikisha wadau wa mpira wa miguu watakaoshauri kuwe na timu ya ushindani itakayocheza fainali za michuano hiyo.
“Tunajua Stars inashiri ya kimataifa, Mwenendo wa timu yetu inajulikana , tunataka tufanye mabadiliko ya haraka tuwe kama Senegal , lazima tuingie katika maandalizi thabiti, tunahitaji kwenda kushinda na kucheza Fainali.
Haipendezi tukawa washangiliaji, tukae nakuangalia nani anaweza kuinoa timu yetu, nini inahitajika pamoja na sehemu au nchini gani ya kuweza kwenda kufanya maandalizi mazuri ya kufanya maandalizi,” amesema Waziri Majaliwa.
Amesema jambo hilo lifanywe haraka kujenga Stars imara, yenye ushindani, Serikali itafanya kazi karibu na kamati na wadau kuhakikisha wanafanikiwa katika mipango mkakati kuelekea AFCON.
Waziri Majaliwa amesema Maandalizi kuelekea michuamo hiyo wamefikia hatua muhimu na anawapongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Hussein Mwinyi.
“Serikali imeanza kujipanga na mashindano ya kufanyika kwa uweledi mkubwa na kufungua fursa nyingine. Kuwepo kwa uwanja vingi, tayari tumeanza ujezi wa CCM Kirumba (Mwanza), Majimaji (Ruvuma), Mkwakwani (Tanga), Jamhuri (Morogoro) na Sokoine (Mbeya).
Kukamilika kwa viwanja itatoa nafasi ya klabu za Tanzania kukaa kokote na kufanya maandalizi kwa kuwa kutakuwa na miundo bora, uwepo wa Kamati hii Serikali ina imani kubwa kuweza kusimamia AFCON na CHAN, September mwaka huu,” anasema Majaliwa.
Ametaja faida ya Tanzania kuwa wenyeji wa mashindano hayo kukaribisha uwekezaji mkubwa hapa nchini kwa mataifa mengine kuja kuandaa mashindano kutokana na ubora wa miundo mbinu.
Majaliwa amesema kamati kuu ziko tatu kamati ya kwanza ya kimataifa inayosimamiwa na Wizara, nyingine makatibu na kamati ya wadau wa soka pia kutakuwa na kamati ya Habari ambayo inatakiwa kufanya kazi mara moja kwa kila siku kutangaza AFCON.
Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt.Damas Ndumbaro ameiomba kamati hiyo kuhakikisha timu ya Taifa Stars inaendelea kufanya vizuri kwenda AFCON ya 2025 nchini Morocco.
Amessma wamekaa na kupanga mkakati yao ni kuona wanapiga ‘Hat Trick’, katika michuano hiyo baada ya kucheza Fainali za 2023 na kutafuta ya pili ya mwaka 2025.
“Naomba niwaongezee jambo moja hii kamati ya maandalizi ya AFCON 2027, wabebe na jukumu la kuhakikisha timu yetu ya Taifa Stars inaenda kucheza fainali ya pili ya michuano hiyo 2025 na 2027 hiyo haina ujanja.
Tumeona kundi la Tanzania kuelekea michuano ya 2025, tukiwa na Congo, Guinea na Ethiopia tunafahamu uwezo wa timu hizo sasa ni wakati wetu wakutafuya mafanikio na kwenda kwenye fainali hizo,” amesema Ndumbaro.
Ameongeza kuwa msimu ulioisha Tanzania ilikuwa kwenye port namba nne, safari hii port namba tatu, wanatarajia kuelekea 2027 wanakuwa port namba mbili na kufanya vizuri katika michuano ya kombe la Dunia.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Leodgar Tenga ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Afcon amesema walipokuwa Misri, walifanya kazi mkubwa ya kupiga kampeni ya kuchagua Tanzania, Kenya na Uganda wanakuwa wenyeji ya mashindano hayo.
“Haikuwa rahisi kwani viongozi walipambana katika kampeni za kuwashawishi watu hadi kuwa wenyeji, pia mimi na mwenzangu tuliochanguliwa tutafanya kile kinachostahili ili kufanya vyema Afcon 2027.
Tuna kazi mkubwa ya kufanya, watu waliopo katika katika kamati hii ni watu wenye uweledi ambao wanaweza kufanya kazi hadi usiku, “amesema Tenga.
Katibu wa BMT, Neema Msitha amesema Tanzania itapata manufaa makubwa katika mashindano hayo ikiwemo kuongezeka kwa mapato ya fedha kufikia dola za kimarekani milioni 180 kwa kila klabu inayoshiriki.
Amesema manufaa mengine timu ya taifa itaimarika baada ya kushiriki mashindano hayo pamoja na vijana kupata ajira za muda fupi.
“Tanzania imepata fursa hii ya kuandaa kutokana na utashi wa kisiasa na utayari wa serikali, mkakati mzuri wa kampeni pamoja na mchakato nzuri wa miundombinu ya viwanja, “amesema .
Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, Wallace Karia amewapongeza Serikali kwa kusapoti wazo na dhamira waliyoitoa kuwa Tanzania kuandaa michuano ya AFCON.
“Tulitoa wazo wazo na Serikali wakalibeba na hadi kufikia kuwa wenyeji wa AFCON, kuna wadau wanatusaidia lakini Serikali inasimamia vema na tunatumia fursa hiyo kuhakikisha tunatekeleza yaliyo mbele yetu ikiwa AFCON,” amesema Karia.