Ligi KuuNyumbani

Mashujaa vs Tabora UTD: Dabi ya majirani

LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa mchezo mmoja kufanyika mkoani Kigoma.

Wenyeji Mashujaa inayoshika nafasi ya 15 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi nane baada ya michezo tisa itaikaribisha Tabora United yenye pointi 14 iliyopo nafasi ya tisa baada ya michezo kumi kwenye uwanja wa Lake Tanganyika.

Katika mchezo mmoja wa ligi hiyo uliopigwa Desemba 4 kwenye uwanja wa Highland Estates, Mbarali mkoani Mbeya, wenyeji Ihefu imelazimishwa suluhu dhidi ya Tanzania Prisons.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button