Filamu

Patrick Stewart afariki, aliliwa kila kona

CALIFORNIA: MWIGIZAJI mashuhuri, Sir Patrick Stewart amefariki akiwa nyumbani kwake Los Angeles baada ya mapambano mafupi ya maradhi ya ‘Alzheimer na Lewy Body Dementia’.

Stewart, 86 raia wa Uingereza alitamba mno kama Kapteni Jean-Luc Picard katika kipindi cha Star Trek: The Next Generation na Profesa Charles Xavier kwenye filamu za Marvel, X-Men.

Kampuni ya Marvel Studios ilieleza kupokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Stewart, aliyeshinda na kutunukiwa tuzo nyingi ikiwemo ya ushujaa aliyopewa na Malkia Elizabeth II mwaka 2010.

“Alikuwa na kipaji cha kipekee, alikuwa mshirika mkarimu, na mtu mwenye heshima na uungwana wa kweli.

“Tunawapa pole sana mkewe Sunny, watoto wake, marafiki zake, pamoja na mashabiki wake wasiohesabika kote duniani ambao maisha yao yaliathiriwa vyema na kazi yake ya sanaa,” ilifafanua taarifa hiyo.

Aidha, siku chache kabla ya kifo chake, mwigizaji mwenzake wa Star Trek, Walter Koenig, aliyeigiza kama Ensign Pavel Chekov, naye alifariki akiwa na umri wa miaka 90.

William Shatner, aliyeigiza pamoja na Stewart kama Kapteni Kirk katika mfululizo wa awali wa Star Trek, alielezea kuwa kipindi hiki ni kama wiki yenye kuvunja moyo.

Mwigizaji, Hugh Jackman aliyevaa uhusika wa Wolverine kwenye X-Men alisema: “Tumepoteza mmoja wa magwiji wa jukwaa na skrini. Kwangu alikuwa rafiki wa pekee na mtu wa ajabu. Nilijifunza mengi sana kutoka kwake. Nitakukumbuka daima Patrick Stewart.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button