Ligi Kuu

Barker: Tuko tayari kukabiliana na changamoto Afrika

DAR ES SALAAM:KOCHA Mkuu wa Simba, Steven Barker, amesema kikosi chake kinakabiliwa na kundi lenye ushindani mkubwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini kimejipanga kupambana ili kufuzu hatua ya mtoano.

Simba imepangwa kundi pamoja na RS Berkane ya Morocco, Orlando Pirates ya Afrika Kusini na Colombe Sportive ya Cameroon, timu ambazo Barker amezitaja kuwa na uwezo wa kuipa changamoto timu yake.

Barker amesema anaifahamu vizuri RS Berkane kutokana na kukutana nayo wakati akiwa Simba katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, pamoja na uzoefu alioupata alipokuwa akiinoa Stellenbosch ya Afrika Kusini.

Amesema pia anafurahia kukutana na Orlando Pirates, ambayo amewahi kukabiliana nayo mara kadhaa alipokuwa akifanya kazi nchini Afrika Kusini, akieleza kuwa ni timu yenye ushindani mkubwa baada ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya nchi hiyo msimu uliopita.

Kuhusu Colombe Sportive ya Cameroon, kocha huyo amesema nayo itakuwa na changamoto yake, licha ya kuwa miongoni mwa timu zinazoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza.

“Ni kundi lenye ushindani mkubwa, lakini kama unataka kufika mbali katika mashindano haya, lazima uvuke hatua ya makundi bila kujali wapinzani unaokutana nao. Tunapaswa kutafuta njia ya kuhakikisha tunafuzu hatua ya mtoano,” amesema Barker.

Amesema kwa ujumla anafurahia changamoto hiyo na anasubiri kwa hamu kuanza kwa michezo ya hatua ya makundi, huku akisisitiza umuhimu wa Simba kufanya vizuri ili kutimiza malengo yake katika mashindano hayo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button