Burudani

P Diddy awajia juu waendesha mashtaka

MSANII wa Muziki wa Hip Hop kutoka nchini Marekani Sean Combs, ‘P Diddy’, amewashutumu mawakala wa shirikisho na waendesha mashtaka kwa kuvujisha taarifa zake kinyume na Sheria Mahakamani.

P Diddy amezuiliwa bila dhamana baada ya kukamatwa na kushtakiwa mwezi uliopita kwa ulanguzi wa ngono kwa nguvu, usafiri wa kujihusisha na ukahaba na kula njama za kulaghai.

Mawakili wa P Diddy wamedai kuwa taarifa hizo zimesababisha kumchafua zaidi staa huyo na huenda mahakama ikashindwa kutoa haki kwa staa huyo.

Wanadai video ambayo ilirushwa hewani na CNN  P Diddy akimshambulia Ex wake anayejulikana kwa jina la Cassie Ventura ilikuwa sehemu ya kampeni iliyoongozwa na serikali ya kuchafua sifa ya Diddy na upendeleo wa maoni ya umma kabla ya kesi yake kusikilizwa.

Related Articles

Back to top button