Ligi KuuNyumbani

Simba ipo Jamhuri Moro, dabi ya kijeshi Kigoma leo

LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea kushika kasi huku baadhi ya klabu zikisaka kutwaa ubingwa, nyingine zikijiweka mazingira mazuri kuingia nne bora lakini nyingine zikitafuta alama muhimu kuepuka kushuka daraja.

Miamba ya Dar es Salaam, Simba iliyopo nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 36 baada ya michezo 15 itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons inayoshika nafasi ya 6 ikiwa na pointi 24 baada ya michezo 18 kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Huko Kigoma kuna dabi ya kijeshi ambapo JKT Tanzania iliyopo nafasi ya 13 ikikusanya pointi 19 baada ya michezo 18 itakuwa mgeni wa Mashujaa inayoshika nafasi ya 14 ikiwa na pointi 18 baada ya michezo 19 kwenye uwanja wa Lake Tanganyika.

Dodoma Jiji iliyopo nafasi ya 12 ikiwa na pointi 20 baada ya michezo 18 itakuwa mwenyeji wa majirani zake Tabora United inayoshika nafasi ya 11 ikiwa na pointi 21 baada ya michezo 19 kwenye uwanja wa Jamhuri.

Nayo Coastal Union iliyopo nafasi ya 4 ikiwa na pointi 26 baada michezo 18 itakuwa mgeni wa Azam inayoshika nafasi ya 2 ikiwa na pointi 43 baada ya michezo 19 kwenye uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button