Ligi Kuu

Mzizima Derby kupigwa usiku kwa Mkapa

DAR ES SALAAM: BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imebadili uwanja na muda wa kuanza kwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Simba SC vs Azam FC ambao awali ulipangwa kupigwa kwenye uwanja wa KMC Complex Jumatatu Februari 24, 2025 kuanzia saa 10:00 jioni.

Taarifa iliyotolewa na bodi hiyo imesema kuwa Mchezo huo sasa utafanyika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kuanzia saa 1:00 usiku siku hiyo hiyo ya Februari 24, 2025.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa sababu ya mabadiliko hayo ni kutoa nafasi kwa mashabiki wengi zaidi kuhudhuria mchezo huo ambao ni moja ya michezo inayovuta hisia za watu wengi.

Related Articles

Back to top button