Afrika Mashariki

Mwanamke anayedai kuwa mke wa Fredi Omond ajitokeza

NAIROBI, Kenya: MWANAMKE anayedai kuwa mke wa Fredi Omondi (marehemu) ambaye ni ndugu wa mchekeshaji Erick Omond amejitokeza huku akiwakaribisha wanawake wengine waliodai kuwa na watoto na mume wake huyo kabla ya kifo chake.

Kujitokeza kwa mwanamke huyo hakukutarajiwa na wengi kiasi cha kubaki wakishangaa kwa kuwa Fred Omondi hakuwahi kumtaja hadharani mke wake.

Katika mahojiano na shirika la habari nchini Kenya mnamo Juni 28, mwanamke huyo, ambaye alichagua kutotaja jina lake, alisema kuwa yeye ni mke wa Fred Omondi na mama wa bintiye wa miaka miwili, Kyla Adhiambo Omondi.

Marehemu Fred alikuwa ametaja kuwa na binti ambaye alimpenda, lakini bado haijulikani ikiwa Kyla ni mtoto aliyetajwa.

Licha ya uhusiano wao, alikuwa amekaa nje ya macho ya umma. “Mimi ni mke wa Fred. Nina mtoto. Ana umri wa miaka miwili na jina lake ni Kyla Adhiambo Omondi,” alisema.

Alipoulizwa kuhusu mapokezi yake na familia ya Fred Omondi, alionyesha shukrani kwa mapokezi hayo mazuri, ambayo yalikuwa kinyume na matarajio yake. Aliogopa kukataliwa kwani ilikuwa ni ziara yake ya kwanza kwa familia ya Fred.

“Nataka kumshukuru mama wa Fred kwa kunikaribisha kwa uchangamfu. Nilipofika nyumbani, nilifikiri wangeniuliza mimi ni nani, lakini dada na ndugu walinikaribisha kwa fadhila zote. Ninashukuru,” alisema.

Mwanamke huyo alisafiri hadi nyumbani kwa Fred Jumapili usiku, akafika Jumatatu asubuhi. Alichagua kuja peke yake kutokana na kutokuwa na uhakika kuhusu mapokezi ambayo angepokea. “Nilisafiri Jumapili usiku na kufika nyumbani Jumatatu asubuhi. Nilikuja peke yangu kwa sababu ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika nyumbani. Sikuwa na uhakika kama ningekaribishwa au kuachwa,” alieleza.

Alifichua kwamba Fred alikuwa ameshiriki naye malezi ya familia yake, akieleza kwamba anataka kuwa na uhusiano wa kifamilia. Hilo lilimchochea kukubali kuwa mke wake, ingawa hawakuishi pamoja. “Fred aliniambia kuhusu historia yake, kwamba hakuwa na wazazi lakini angependa mtu aonekane kama mama. Nilikubali kuwa mke wake. Ingawa hatukuishi pamoja, ningemtembelea kwa takriban mwezi mmoja kabla ya kurudi nyumbani kwangu,” alisema.

Alieleza wakati alipopokea taarifa za kifo cha Fred Omondi, akielezea kutokuamini, alipatwa mstuko mno. “Fred alikuwa na furaha kila wakati. Sikuwahi kuona jambo lolote baya kumhusu. Tulikuwa sawa. Asubuhi moja, rafiki yangu alinipigia simu na kusema Fred alikuwa katika Hospitali ya Mama Lucy, lakini sikuamini. Nilikuwa nimetoka kuongea naye, akasema anakuja kumuona mtoto wetu kwa sababu nilikuwa nyumbani kwa mama yangu huko Kibera. Nilienda katika Hospitali ya Mama Lucy lakini bado sikuamini hadi nikagundua kuwa tayari alikuwa ameaga dunia na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti,” aliongeza.

Katika taarifa yake ya ajabu, alionyesha nia yake ya kuwakubali wake wenzake kama wangekuwepo. “Sina hakika kama kuna wengine, lakini ikiwa wapo, ninawakaribisha.”

Omondi aliongeza kuwa yuko tayari kuwatunza watoto hao, lakini iwapo tu wanafanana na Fred Omondi. “Kuna watoto nyumbani wanaofanana na Mulamwah. Wale wanaodai kuwa na watoto wa Fred wanapaswa kuhakikisha wanafanana na Fred. Wawili tayari wamefika nyumbani,” Eric alisema.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button