Muziki

Wasanii wa injili wapongezwa

DAR ES SALAAM: Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama, amewapongeza wasanii wa nyimbo za Injili kwa kuandaa wimbo wa kuhamasisha amani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, February 27, 2025 katika uzinduzi rasmi wa Tuzo za Muziki wa Injili Afrika Mashariki, Msama amesema kuwa tuzo hizo zitaleta chachu katika tasnia ya muziki wa Injili na kusaidia kukuza pato la taifa, kwani muziki huo unazidi kufanya vizuri katika kanda ya Afrika Mashariki.

“Ni muhimu kwa waimbaji wa nyimbo za Injili kuendelea kuachia nyimbo zinazoimiza amani, umoja, na mshikamano.

Pia, wanapaswa kuwa mstari wa mbele kuhamasisha Watanzania kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwa amani na utulivu ili tupate viongozi waadilifu na wachapakazi kwa maendeleo ya taifa,” alisema Msama.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Kedmon Mapana, amewapongeza waimbaji wa nyimbo za Injili kwa mshikamano wao na juhudi za kuandaa tuzo hizo.

“Nimefurahi sana na nawapongeza waandaaji wa tuzo hizi, kwani zitaleta msukumo mpya katika kutunza na kukuza muziki wa Injili, si tu nchini, bali pia kimataifa,” amesema Mapana.

Naye Rais wa Chama cha Waimbaji wa Nyimbo za Injili Tanzania, Ado Novemba, amewataka wasanii wa Injili kuendelea kufanya kazi bora ambazo zitazidi kuleta ushindani katika tasnia hiyo na kutangaza injili kwa viwango vya juu zaidi.

Related Articles

Back to top button