Mrembo wa Big Brother Naija aikana ndoa
LAGOS: MWIGIZAJI nyota wa kipindi cha Big Brother Naija, Doyin David, amesema huwa anaingia kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa sababu ya starehe na uchumba tu siyo kwa ajili ya ndoa.
Doyin amefichua hayo wakati wa mahojiano yake ya hivi karibuni na mwanahabari, Olufemi Daniel.
Akizungumzia uhusiano na mtazamo wake, ameeleza kuwa ndoa sio muhimu kwake.
“Sijawahi kuchumbiana ili niolewe, mimi huchumbiana kwa ajili ya uchumba tu ila siyo ndoa.
“Namaanisha mapenzi ni sehemu kubwa kwangu, lakini siyo kuolewa. Mimi huchumbiana kwa ajili ya kufurahia tendo la ndoa hivyo kama ndoa haitokuwepo wala sina tatizo kwa sababu sifikirii ndoa katika Maisha yangu.
“Ila uhusiano kwangu ni muhimu mno. Kwa hivyo nataka tu kuwa na mtu ambaye ni mtu wangu kwa maisha yangu yote lakini sio muhimu kuolewa,” ameeleza mrembo huyo wa Big Brother.