Mastaa

Miss ‘USA’ awavuruga mashabiki

MAREKANI: UAMUZI wa Noelia Voigt kuachia taji lake la Miss USA umezua wasiwasi miongoni mwa mashabiki wake mtandaoni baada ya mashabiki hao kugundua kitu kisicho cha kawaida juu ya taarifa yake ya kujivua taji.

Voigt, ambaye alitunukiwa taji la Miss USA mnamo Septemba 2023, alitangaza katika taarifa yake katika mtandao wa Instagram Jumatatu kwamba ameamua kujiuzulu na kuandika, “Katika maisha, ninathamini sana umuhimu wa kufanya maamuzi ambayo yanahisi bora kwako na afya yako ya akili”

Lakini katika ‘comments’ za chapisho lake hilo na maeneo mengine kwenye mitandao ya kijamii, watumiaji waligundua kuwa ukichukua herufi ya kwanza katika kila sentensi ya taarifa hiyo unapata neno “I’m silenced” kumaanisha “nimenyamazishwa”. Bado haijafahamika mara moja kama aliandika hivyo kwa makusudi

Katika mtandao wa TikTok moja ya mtumiaji AnnaNoel alisemakuwa mlimbwende huyo Voigt “anajaribu kutuambia jambo muhimu” na “maneno hayo ya siri,” akisema, “sidhani kama hii ni bahati mbaya. … Kuweka kwake ndani ilikuwa hivyo. mtu angejua na mtu angeweza kusikiliza kwa karibu.”

Related Articles

Back to top button