Ligi KuuNyumbani

Mgunda kuteta na mabeki

KOCHA Mkuu wa Simba, Juma Mgunda ataitisha kikao cha dhararu na safu ya ulinzi ya kikosi chake ili kurekebisha makosa yanayojirudia katika mechi za klabu hiyo.

Simba ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Mbeya City Novemba 23 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara na baadaye Mgunda kusema safu ya ulinzi ilifanya makosa na kusababisha wenyeji kusawazisha bao.

Akizungumza na SpotiLeo, kocha huyo amesema anafanya hivyo kutokana na makosa yanayoigharimu na kuiweka timu katika wakati mgumu kwenye mbio za ubingwa.

Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda.

“Nataka tuzungumze na wachezaji wangu na kuelekezana mambo muhimu namna ya kupunguza makosa ili tuweze kulinda ushindi wetu na tusiruhusu mabao kwenye mechi za ligi sababu kama tutaendelea kufanya hivyo itakuwa ngumu kufikia malengo,” amesema Mgunda.

Amesema hawalaumu sababu hakuna mchezaji anayekusudia kukosea, anachotaka ni umakini kuongezeka wanapokuwa mchezoni.

Related Articles

Back to top button