Burudani

Mchekeshaji nguli Malaysia aachwa bila kuelezwa sababu na mkewe

MALAYSIA: MKE wa mchekeshaji nguli vichekesho nchini Malaysia, Harith Iskander, Jezamine Lim amewasilisha kesi ya talaka mahakamani baada ya miaka 14 ya ndoa yao lakini amekataa kueleza sababu za kufanya hivyo.

Mwanamke huyo ambaye ni mjasiriamali wa masuala ya tiba alifika mahakamani hapo akiwa amevalia vazi na hijabu akiwa na wakili wake Abdul Kadir.
Iskander mwenye miaka 58 na Lim mwenye miaka 41, walifunga ndoa mwaka 2010, wana watoto watatu wenye umri wa miaka 14, 11 na mwingine miaka tisa.

Mke huyo Lim alipohojiwa alithibitisha kuwa amewasilisha ombi la talaka mahakamani hapo tangu Juni lakini akakataa kufichua sababu zake.
Iskander, anayejulikana kama baba wa uchekeshaji nchini Malaysia naye alichagua kutotoa maoni kuhusu hilo zaidi ya kushangazwa na uamuzi aliochukua mke wake. “Sina maoni juu ya suala hilo,” alisema.

Vyanzo vya habari vinaripoti kwamba kesi ya talaka itatajwa mahakamani mwezi huu, kama ilivyobainishwa na The New Straits Times la nchini humo.

Related Articles

Back to top button