Mashauzi asimama na Mama ntilie
Msanii wa Taarabu Isha Mashauzi ‘Jike la Simba’ ameomba wanawake mama ntilie waangaliwe kwa jicho la tofauti katika kupatiwa mikopo ya kujikimu na biashara zao.
Akizungumza na Spotileo leo jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa Malkia choice FM yenye lengo la kusaidia wanawake, Isha amesema amefurahishwa na kipindi hicho kwani kitaleta tija kwa wanawake.
“Mwanamke ni kiungo kikubwa chenye vitu vingi ila ombi langu ni kwa wanawake wajasiliamali wanaopika wapewe mikopo itakayosaidia kukuza biashara zao,”amesema Isha.
“Binafsi ni miongoni mwao,mimi ni Mpishi, napika hivyo naelewa changamoto za biashara hasa kwenye suala la mtaji kama haupo vizuri inapelekea biashara kuyumba kitu ambacho sio kizuri. Kumbuka Mama anapambana familia iweze kula na kupeleka watoto shule hivyo wanahitaji kutazamwa kwa jicho la kipekee ili waweze kuzihudumia jamii na familia zao”amesema Isha.