Tetesi
Man Utd yamweka sokoni Sancho

KLABU ya Manchester United inakusudia kumuuza Jadon Sancho huku Aston Villa ikionesha nia kumsajili.
Kwa mujibu wa mtandao wa Football Transfers baada ya kutumikia kwa miaka miwili winga huyo sasa anaruhusiwa kuondoka Old Trafford.
Man Utd inataka ilipwe pauni milioni 60 sawa na shilingi bilioni 176 kwa ajili ya Sancho.
Kwa sasa Villa haina mpango wa kumnunua muingereza huyo kwa kiasi hicho cha fedha lakini majadiliano yanaweza kufanyika vizuri na makubaliano kufikiwa kati ya pande hizo mbili.
Sancho amefunga mabao 12 na kusaidia mara sita katika michezo 79 aliyocheza Man Utd.