Tetesi

United yasaka mbadala wa Casemiro

TETESI za usajili zinasema Manchester United inamlenga kiungo wa Wolves Joao Gomes, 23, awe mbadala wa mbrazil mwenzake Casemiro, 32. (Mirror)

Liverpool inapanga kuwaruhusu beki wa zamani wa Cameroon Joel Matip, 32, kiungo wa zamani wa Hispania Thiago Alcantara, 32, na golikipa wa kihispania Adrian, 37, kuondoka majira yajayo ya kiangazi. (Football Insider)

Matumaini ya klabu ya Getafe ya Hispania ya kumsajili kwa mkopo tena fowadi wa England Mason Greenwood, 22, msimu ujao huenda yakayeyuka kutokana na Manchester United kutaka dili la kudumu iwapo itataka kumruhusu kuondoka. (Sun)

Barcelona inakusudia kuipatia Everton ofa ya wachezaji wanne- winga mhispania Ansu Fati,21, beki wa kati wa kifaransa Clement Lenglet,28,  beki wa kulia wa Marekani Sergino Dest,23, na kiungo mhispania Fermin Lopez,20, katika ombi lao la kumsajili kiungo wa Senegal, Amadou Onana, 22 anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni mil 80. (Sport via Teamtalk)

Kiungo mholanzi Teun Koopmeiners ameiambia klabu yake ya Italia, Atalanta kwamba anataka kuondoka majira yajayo ya kiangazi, huku mdachi huyo mwenye umri wa miaka 26 akihusishwa na Liverpool. (Metro)

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button