Liverpool: Mo Salah hauzwi
LIVERPOOL imeng’ang’ania msimamo wake kwamba mchezaji nyota Mohamed Salah hauzwi majira haya kiangazi, licha ya kuendelea kwa juhudi za klabu ya Al-Ittihad ya Saudi Arabia kutaka kumsajili Mmisri huyo kwa mkataba wa fedha nyingi.(Daily Mail)
Kylian Mbappe amekataa ofa ya hivi karibuni ya mkataba Paris Saint-Germain na bado ana mipango kuondoka klabu hiyo akiwa huru majira yajayo ya kiangazi ili ajiunge na Real Madrid.(Marca)
Tottenham Hotspur iko katika mazungumzo na Nottingham Forest kuhusu fowadi wa Wales, Brennan Johnson ambaye gharama yake inaonekana kuwa tatizo.(Independent)
Johnson pia inaivutia Chelsea ambako maafisa kadhaa wa klabu hiyo wanasemekana kuwa mashabiki wakubwa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22.(football.london)
Manchester City inaandaa ofa ya pili kwa ajili ya kumsajili Matheus Nunes wa Wolverhampton Wanderers baada ya ofa ya kwanza ya pauni milioni 47 kukataliwa.(Telegraph)
Chelsea iko katika mazungumzo kuhusu kumpeleka Romelu Lukaku katika klabu ya Roma kwa mkopo lakini Barcelona na PSG zinaweza kushindana kumsajili iwapo mbelgiji huyo atapatikana kwa dharura.(Gianluca Di Marzio)
Bado kuna mipango kwa Manchester United kusajili mshambuliaji mwingine kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa huku Marcos Leonardo kutoka Santos mwenye umri wa miaka 20 akipewa kipaumbele katika orodha ya wanaopendekezwa.(Gazzetta dello Sport)
Arsenal na Tottenham zote zina nia ya kumsajili mshambuliaji wa Brentford, Ivan Toney, ambaye atakuwa na thamani ya pauni milioni 80 mara kifungo cha makosa ya kushiriki kamari kitakapoondolewa Januari, 2024.(Times)
Liverpool ina nia ya kutuma ombi la kumsajili winga Federico Chiesa wa Juventus kwa pauni milioni 43, lakini timu hiyo ya Italia imeng’ang’ania kuwa bei ya mchezaji huyo ni pauni milioni 51.(TuttoJuve)