Tetesi
Man Utd yakaribia kunasa saini ya Onana

BAADA ya ofa kadhaa za Manchester United kumsajili golikipa wa Inter Milan, André Onana kukataliwa, mashetani hao wekundu wametoa ofa nyingine yenye thamani ya euro milioni 50 sawa na shilingi bilioni 129.65 pamoja huku nyongeza ya euro milioni 5 sawa na shilingi bilioni 12.96 pia ikijadiliwa.
Tovuti ya michezo espn ya Hispania imesema vipengele binafsi na Golikipa huyo wa kimataifa wa Cameroon mwenye umri wa miaka 27 ambaye amewahi kuwa chini ya kocha wa sasa wa United, Erik ten Hag katika timu ya Ajax vimekubaliwa.
Onana alikuwa katika kiwango bora Inter msimu uliopita akicheza michezo 41 katika mashindano yote ikiwemo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya klabu hiyo ilipopoteza mbele ya Manchester City.