Mamba: Wasanii tuimbe kuelimisha jamii
MSANII Iwa muziki wa Singeli Jumuiya Abdallah ‘Mamba Kisingeli’ amehimiza wasanii wenzake waimbe muziki kwa ajili ya kuelimisha jamii.
Akizungumza na SpotiLeo nyota huyo amesema kwa kuimba nyimbo za kuelimisha kutasaidia kuiweka jamii salama kimaadili.
“Wasanii tuimbe nyimbo za kuelimisha jamii ili kuhakikisha jamii inakuwa kwenye mstari ulionyooka na yenye maadili kwa kuwa nyimbo za singeli zinajukumu na kuiongoza jamii,”amesema.
Mamba ametambulisha wimbo wake mpya uitwao, Moyo aliomshirikisha Msanii Fadhili Chunchu na kuomba mashabiki zake kumsapoti kwani tayari ameupakia katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
Wimbo huo wa mapenzi umerekodiwa studio ya Vinanda ya Chamanzi, Dar es Salaam.
Mbali na wimbo huo Mamba pia, amewahi kuimba nyimbo nyingine nyingi kama vile Madolali, Dua, Najali, Zamu ya umeme,Tutoke na Zuena aliomshirikisha msanii Msaga Sumu