Burudani

Paulina Onna: Siwezi kumchagulia kazi mwanangu

MKE wa msanii Dogo Janja anayejulikana kwa jina la Paulina Onna maarufu ‘Quenlinnatotoo’amesema baada ya kupata mtoto wa kiume ‘Ahyan’ amesema kamwe hawezi kumchagulia kazi ya kufanya mtoto wake atakapokuwa.

Akipiga stori na SpotiLEO, mwandishi wa mtandao huu alitaka kujua iwapo mtoto huyo atafuata kazi ya muziki ya baba yake au uongozi wa kampuni kazi ya mama yake ambapo Quenlinnatotoo alisema mtoto huyo ataamua mwenyewe nini atapenda kufanya.

“Mwanangu afanye kazi ya baba yake au kazi yangu sitakuwa namtendea haki Mungu ndiye anayejua alichompangia, hivyo atakachopenda mimi kama mama yake nitamsapoti atapohitaji awe nani na nitamwelekeza vizuri mtoto wangu,” amesema Quenlinnatotoo.

Amesema baada ya kupata mtoto huyo hafikirii kuishia hapo kwani bado ana safari ya kuendelea kupata watoto wengine na mume wake ‘Janjaro’.

“Idadi ya watoto sina hesabu ninazoweza kukupa napenda watoto nalea watoto wengi zaidi, ninao mpango wa kuongeza mtoto mwingine huko mbeleni na mume wangu,” ameiambia SpotiLEO.

Related Articles

Back to top button