Nyumbani

‘Mama’ aupiga mwingi hadi COSOTA

DAR ES SALAAM: AFISA Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki (COSOTA), Doreen Anthony amesema wamepiga hatua kubwa ndani ya miaka mitatu ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Doreen amewaeleza waandishi wa habari kuwa wamepata mafanikio hayo katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Dr Samia ikiwemo suala la maboresho katika sheria, ikiwemo Serikali kusikiliza wadau katika mgao wa mirabaha pamoja na kutoa leseni kwa makampuni ya muziki.

Amesema Serikali imewaweza kutoa elimu kwa wadau, elimu ambayo inawanufaisha katika kuongeza kipato lakini pia wasanii kuwa na ubunifu katika kazi zao kwani sanaa ni ajira kubwa nchini.

pamoja na hayo Afisa mtendaji mkuu huyo amewaambia waandishi wa habari jinsi uongozi wa Dr Samia ulivyoiwezesha COSOTA kufanya kazi mbalimbali ikiwemo kusaidia uchapishaji wa vitabu kuwasaidia watu wenye uoni hafifu, kuongeza ushirikiano na mamlaka za hakimiliki za mataifa mengine pamoja na kuongeza mapato yaliyosaidia wao kutoa mirabaha kwa wasanii ikiwa ni kwa mara ya kwanza nchini

“COSOTA kupitia Serikali tumeweza kusaidia kwa watu wenye uoni afifu, kupata machapisho na vifaa maalum zilianza katika majaribio na kuonekana kusaidi, ndani ya miaka mitatu hii kumeongezeka ushirikiano wa mataifa mengine kwenye masuala ya haki miliki.

Kuongeza kwa mapato kwa kukusanya zaidi ya sh milioni 700 kati ya fedha hizo asimilia 10 zilienda TRA, Wizara ya Utamadauni na Sanaa pamoja na wasanii katika mgao wa mirahaba,” amesema Doreen.

Ameeleza kuwa wanatarajia mwaka huu kuongezeka kwa mapato lakini pia kuboresha mfumo wa ubunifu kuweza kuingiza katika mfumo wa kujisajili kuingia katika mfumo pamoja na kuweka katika bajaeti na kujisimamia.

Related Articles

Back to top button