Tetesi

Madrid, Bayern, PSG zamfuatilia Vlahović

Real Madrid, Bayern Munich, Paris Saint-Germain na vilabu mbalimbali vya Ligi Kuu England vinafirikia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji Dušan Vlahović wa Juventus, umesema mtandao wa michezo, Calciomercato wa Italia.

Wakati hatma ya Vlahović katika klabu ya Juve haina uhakika, Vlahović anaweza kucheza klabu nyingi, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Serbia sio kipaumbele cha timu yoyote kati ya hizo.

Juventus iko tayari kumruhusu mchezaji huyo wa zamani wa Fiorentina kuondoka lakini timu itanomhitaji italazamika kulipa ada ya Euro milioni 90 sawa na shilingi bilioni 229.7.

Bayern imemfikiria Vlahović baada ya mipango ya kumsajili Harry Kane wa Tottenham Hotspur na Randal Kolo Muani kushindwa lakini kipaumbele kinabaki kwa Kane.

Chelsea, Manchester United, Tottenham na Arsenal zimeonesha nia kwa Vlahović lakini hakuna iliyochukua hatua.

Atletico Madrid na Real Madrid pia zimetajwa huku Vlahović akionekana kuwa mbadala wa Kylian Mbappé wa Paris Saint-Germain ambaye amekataa kuongeza wake wa sasa unaomalzika 2024.

Related Articles

Back to top button