Mastaa

Paul wa Psquare: Unapopata pesa oa mwanawake tajiri

LAGOS: MWIMBAJI maarufu kutoka kundi la PSquare, Paul Okoye maarufu Rudeboy, amewashauri wanaume kufanya kazi kwa bidii ili kupata pesa na wanapopata hizo pesa waoe wanawake matajiri.

Paul amesema wakati wakuoa waznaume wanatakiwa wazingetie kutimiza malengo yao yote waliyojioangia katika Maisha yao.
Paul amesisitiza kwamba kiwango cha fedha ambacho wanawake wanaomba wanapokuwa katika uhusiano na wanaume kabla hawajaingia katika uhusiano ndoa ni kikubwa mno kiasi cha kutisha.

Mkali huyo wa ‘Reason with Me’ amewataka wanaume wanaohangaika kusaka maisha kwa kutumia nguvu nyingi wakipata pesa zao wasione haya kuoa wanawake wenye fedha kwa maana baada ya kupata fedha wanatakiwa wfurahia Maisha na kujenge familia.

Katika akaunti yake ya Instagram, Rudeboy ameandika kwamba, “Wanaume wanatakiwa wawe na fedha wanaume lazima wawe na kiwango kizuri kifedha ndiyo maana wakiangaika kupata pes ani bora waendelee kuoa wanawake wenye pesa.”

“Wanaume badilisha simulizi ya Maisha yako kwa kutafuta pesa kwa hali zote na ukipata pesa tafuta mwanamke tajiri oa,” ameandika Paul.

Related Articles

Back to top button