Tetesi

Liverpool yatupa ndoana kwa Szoboszlai wa Leipzig

KLABU ya Liverpool ipo katika mazungumzo na RB Leipzig kuona uwezekano wa kumsajili Dominik Szoboszlai kutoka timu hiyo ya Ujerumani.

Kiungo huyo wa Hungary mwenye umri wa miaka 22 amesaidia Leipzig kumaliza nafasi ya tatu katika Bundesliga na kutwaa ubingwa wa Kombe la Ujerumani msimu uliopita.

Kwa mujibu wa tovuti ya michezo The Athletic mkutano umefanyika kati ya wawakilishi wa kambi ya Szoboszlai
na Liverpool ambayo inaangalia kuimarisha safu ya kiungo.

Kuna habari kuwa Szoboszlai ana kipengele cha kuachiwa chenye thamani ya karibu pauni milioni 60 sawa na shilingi bilioni 177.27.

Szoboszlai amecheza mechi 31 za Bundelsiga akiwa Leipzig msimu uliopita akifunga magoli sita na kutoa pasi nane za magoli.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button