Nyumbani
Ligi U17 kuanza Machi

LIGI ya mpira wa miguu ya U17 inatarajiwa kuanza mwezi ujao.
Taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imesema: “Klabu za Ligi Kuu ya NBC na Klabu za Championship zinatakiwa kuthibitisha ushiriki ligi ya U17 2024.”
Mwisho kwa timu kuthibitisha kushiriki ni Februari 9, 2024.