Nyumbani

Jeshi la Simba Msimu ujao

DAR ES SALAAM: KATIKA kikosi cha wachezaji 30 cha Simba waliotambulishwa rasmi kwa ajili ya msimu wa 2024/25 wa mashindano, nyota wawili wamekosekana ambao ni Kiungo Mshambuliaji Willy Onana na golikipa Aishi Manula

 

Nyota hao 30 ni makipa m watano;Hussen Abel, Ally Salim, Ayoub Lakred, Ally Ferouz na Moussa Camara ambaye ni usajili mpya kutoka Horoya AC ya Guinea.

 

Imeelezwa kuwa Simba wamemuuza Onana kwa klabu ya Muaither ya nchini Qatari, wakichukua dola za kimarekani 100,000 na 150,000 kwenda kwa mchezaji huyo ambaye nafasi yake ya mchezaji wa kigeni imechukuliwa na kipa kutoka Horoya AC ya Guinea.

 

Kwa upande wa kipa Aishi Manula,yeye alisahulika kwenye utambulisho wa nyota hao waliokuwepo uwanja wa Benjamin Mkapa.

 

Wachezaji wengine waliotambulishwa na Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally ni Mohammed Hussein, Shomari Kapombe, Che Malone Fondoh na Joshua Mutale atakayevaa jezi namba 7.

 

Deborah Fernandes akiwa na jezi namba 17 ambayo alikuwa akivaa Clatous Chama aliyesajiliwa na Yanga, Steven Mukwala akivalia jezi namba 11 aliyokuwa akivaa Luis Miquisson na Jean Charles Ahoua aliyepewa jezi namba 10 aliyokuwa akivaa Said Ntibazonkiza.

 

Wachezaji wengine wanaokamilisha orodha hiyo ni Mzamiru Yassin, Freddy Michael, Karaboue Chamou, Fabrice Ngoma, Edwin Balua, David Kameta, Augustine Okejepha, Valentino Mashaka, Salehe Karabaka, Kelvin Kijili, Abdulrazack Hamza, Awesu Awesu, Yusuph Kagoma, Hussein Kazi, Omary Omary, Valanten Nouma, Kibu Denis na Ladack Chasambi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button