Ligi Daraja La Kwanza

Kitambi: Ubutu umetushusha daraja

KOCHA Mkuu wa Geita Gold, Denis Kitambi amesema ubutu wa safu ya washambuliaji ya timu hiyo ni sababu za kushuka daraja na kucheza Championship msimu ujao.

Akizungumza na Spotileo, Kocha huyo amesema Geita Gold inajipanga kufanya maboresho ya kikosi chake ikiwemo kusajili wachezaji wenye kiwango bora hasa washambuliaji kukabili kugumu wa ligi ya Championship ili kuirejesha timu Ligi Kuu Bara.

“Ni muda wa kukaa na viongozi kuwapa mpamgo Mkakati juu ya msimu ujao tunaenda vipi katika ligi ya Championship, tumeshuka daraja kutokana na aina ya wachezaji tuliokuwa nao hasa safu ya ushambuliaji,”amesema Kitambi.

Kocha huyo amesema Geita Gold ilikuwa ikifikika eneo la wapinzani lakini washambuliaji wanashindwa kumalizia nafasi tunazopata.

Ameongeza kuwa anakabidhi mapendekezo ya aina ya wachezaji anaowahitaji kuelekea msimu ujao wa ligi ya Championship.

Geita Gold imeshuka daraja baada ya kushindwa kupata pointi tatu mbele ya Azam katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu kwa kukubali kipigo cha mabao 2-0 kwenye uwanja wake wa nyumba wa Nyankumbu.

Timu hiyo ilipanda daraja mwaka 2021 pamoja na Mbeya Kwanza ambayo ilicheza msimu mmoja na kushuka daraja.

 

Related Articles

Back to top button