Europa

Kiko wapi Xabi Alonso?

Huenda sifa zote zikamuangukia Staa wa mchezo wa fainali ya ligi ya Europa, Ademola Lookman baada ya kufunga mabao matatu na kuiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa michuano hiyo mikubwa.

Lakini Uwezo wa kocha wa timu hiyo,Gian Piero Gasperini hauwezi Kufichwa na hii ni baada ya kazi ngumu ya kumfunga Bingwa wa ligi kuu ya Ujerumani ambaye hakupoteza mchezo hata moja toka msimu huu ulivyoanza.

Sio kazi rahisi kumzidi mbinu Xabi Alonso ambaye alifanya timu yake kuwa tishio barani Ulaya baada ya kucheza michezo 51 pasi na kupoteza mchezo wowote.Ugumu unakuja zaidi pale ambapo timu hiyo kutoka Ujerumani ilikuwa ni tishio katika safu ya ushambuliaji kwani iliweza kufunga magoli 143 na kuruhusu 42 tu.Lakini Gian Gasperini aliweza kuja na mbinu zilizoiwezesha timu hiyo kupata mabao matatu tena bila kuruhusu goli dhidi ya timu ambayo imefanya ‘comebacks’ kwenye zaidi ya michezo 15 msimu huu ikipata matokeo dakika za jioni.

Gian Gasperini alianza kuinoa timu ya Atalanta toka mwaka 2016 na kwa hakika,licha ya kuwa na wachezaji wa kawaida sana,ameweza kuifanya timu hii kushindana nguvu na vinara wa ligi ya Seria A.

Aliiwezesha Atalanta kumaliza katika nafasi ya 3 kwenye msimamo wa Seria A kwa misimu mitatu mfululizo(2019-21)

Huu unakuwa ubingwa wa kwanza kwa Atalanta katika historia ya klabu hiyo yenye miaka 116.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button