Europa

Guardiola anang’ata na kupuliza

KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola anaamini kuwa Real Madrid watalipiza kisasi katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya leo usiku.

Msimu uliopita City iliifunga Real 5-1 katika michezo miwili ya nusu fainali ligi hiyo msimu uliopita.

Hata hivyo, Guardiola hana shaka kwamba washindi hao mara 14 watakuwa na mtihani mgumu katika hiyo kwani Manchster City pia wamedhamiria kufanya vizuri.

“Ni vigumu sana kwa jambo hilo hilo kutokea tena kuifunga Real Madrid mara mbili mfululizo haiwezekani. Wamejifunza na watataka kulipiza kisasi,”amesema Guardiola.

Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti anataka kikosi chake kioneshe nguvu zaidi kiakili kuliko ilivyokuwa wakati timu hizo mbili zilipokutana msimu uliopita.

“Tulicheza bila ujasiri, bila utu,” Ancelotti alisema. “Ujasiri na utu ni jambo la msingi katika mchezo wa aina hii, Jambo muhimu ni kuwa katika ubora wetu, nyanja ya kiakili ni muhimu sana,” amesema Ancelotti.

Related Articles

Back to top button