Masumbwi

Juma Choki kukiwasha leo Saudia Arabia

BONDIA Juma Choki anatarajia kupanda ulingoni leo jioni dhidi ya bondia wa Ufilipino Bryx Piala hatua ya 32 bora mashindano ya ngumi ya dunia yanayofanyika Riyadh, nchini Saudi Arabia.

Choki ametuma video kuomba Watanzania kumuombea dua ili aweze kufanya vizuri na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania.

“Tayari nimefika Saudia Arabia, kikubwa naomba sapoti zenu za dua kama ndugu yenu naamini nitafanya vizuri,”alisema Choki ambaye amesema pambano lake litakuwa la raundi sita.

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limemtakia kila la heri bondia huyo kuhakikisha anawakilisha vizuri.

Takwimu za mtandao wa Boxrec zinaonesha Juma Choki hilo litakuwa ni pambano lake la pili la kimataifa baada ya kuwahi kucheza moja Dubai dhidi ya bondia Abdulaziz Ssebulime wa Uganda na kushinda.

Juma Choki amecheza jumla ya mapambano 10 na kati ya hayo ameshinda tisa na kupata sare moja anakutana na mpinzani ambaye pia, amecheza mapambano 11 na kati ya hayo ameshinda tisa na kupoteza mawili.

Related Articles

Back to top button