Bundesliga
Jude anukia Madrid

IMERIPOTIWA kuwa Real Madrid inakaribia kukamilisha usajili wa kiugno wa Borrusia Dortmund na Taifa la England, Jude Belligham.
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari anayeaminika kwa taarifa za michezo, Fabrizio Romano ameeleza kuwa timu hizo zipo hatua za mwisho za uhamisho huo.
Amesema kuwa makubaliano baina ya mchezaji na Madrid yameafikiwa.
Ameeleza kuwa umeandaliwa mkutano baina ya timu hizo kwa lengo la kukamilisha uhamisho huo ambao unategemewa kuwa mwezi huu.